Parliament of Tanzania

TANZIA

MAREHEMU KASUKU SAMSON BILAGO

(02.02.1964 – 26.05.2018)

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Y. Ndugai (Mb), anasikitika kutangaza kifocha Mbunge wa Jimbo la Buyungu Mkoani Kigoma, Mhe. Kasuku Samson Bilago aliyefariki leo majira ya saa 9 alasiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mhe. Bilago alihamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tarehe 22 Mei,2018 akitokea Hospitali ya DCMC iliyoko eneo la Ntyuka Jijini Dodoma alikokuwa amelazwa awali.Mwili wa Marehemu Mhe. Bilago unatarajiwa kuagwa Bungeni Dodoma siku ya Jumatatu tarehe 28 Mei, 2018 na baadae kupelekwa Kankonko Mkoani Kigoma kwa ajili ya mazishi.

Ofisi ya Bunge inaendelea kuratibu taratibu za mazishi kwakushirikiana na familia ya Marehemu na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's