Parliament of Tanzania

Spika atoa wito kwa watanzania kusajili laini zao mapema

SPIKA wa Bunge Mhe. Job Ndugai amewataka Watanzania kujitokeza kusajili laini zao mapema kwa kutumia mfumo wa kielektrioniki ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza baada ya muda kuisha.

Mhe. Spika alitoa wito huo Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea mabanda ya kampuni mbalimbali za simu ambazo zilisogeza huduma hizo bungeni ili kuwezesha wabunge na watendaji mbalimbali kusajili laini zao za simu bila usumbufu

Alisema Watanzania wanapaswa kuhakikisha wanajiandikisha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ili wapate vitambulisho au namba zitakazowawezesha kusajili laini zao za simu kwa kutumia mfumo wa kielektrioniki.

“Mimi nimeshatoka kujiandikisha kwa kutumia kitambulisho cha NIDA hivyo watanzia wajiandikishe mapema badala ya kusubiri hadi muda uishe ifikapo Desemba 31. Hii itapunguza uhalifu kwa njia ya mtandao kwa kiasi kikubwa,”alisema.

Aidha, alisema hakuna Mbunge yoyote ambaye atashindwa kusajili laini yake ya simu kwa kutumia alama za vidole kwa kampuni anayoitaka.

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's