Parliament of Tanzania

Procedures to Visit the Parliament

Bunge ni Chombo cha uwakilishi wa Wananchi kama Ibara ya 62 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inavyotumika:

“Kutakuwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambalo litakuwa na sehemu mbili, yaani Rais na Wabunge. Rais kama sehemu moja ya Bunge atatekelezza yote aliyokabidhiwa na katiba hii. Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii”

Kimsingi, Bunge ni chombo cha uwakilishi wa wananchi. Kwa kuwa haiwezekani wananchi wote kukusanyika mahali pamoja na kufanya maamuzi muhimu katika uendeshaji wan chi, uwakilishi hauna budi kuwepo. Hii inamaanisha kwamba Wabunge wanapokuwa Bungeni hutekeleza majukumu yao kwa niaba ya wananchi.

Ofisi ya Bunge, kwa kutambua hilo imeweka utaratibu ambapo jamii huruhusiwa kushuhudia namna ambavyo wawakilishi wa wananchi wanavyotekeleza majukumu yao.

Wageni Bungeni

Bunge hufanya mikutano yake mara nne kwa mwaka mjini Dodoma. Wakati wa mikutano hiyo, watu mbali mbali huruhusiwa kutembelea Bunge na kujionea jinsi linavyoendesha shughuli zake. Kanuni ya 136 (1) ya Kanuni za kudumu za Bunge inaeleza ifuatavyo:

“Wageni wanaweza kuruhusiwa kuingia kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Bunge katika sehemu yoyote ya Ukumbi huo ambayo itatengwa kwa ajili yao”

Utaratibu wa kutembelea Bunge upo wazi ambapo watu binafsi, Vikundi, watumishi wa Taasisi za Serikali, Mabalozi wanaowakilisha mataifa yao nchini, Mashirika ya Kidini, Asasi za Kiraia, Taasisi za Kijamii, Wanafunzi (Shule za Awali, Msingi, Sekondari na Vyuo vya Elimu ya Juu) na Wageni kutoka Mabunge nje ya Tanzania au Taasisi za Kimataifa hutumia fursa iliyopo kutembelea Bunge na kuona jinsi linavyoendesha shughuli zake.

Utaratibu wa Kufuatwa

Utaratibu mzuri unaopaswa kufuatwa na wanaotaka kutembelea Bunge ni kuandika barua ya maombi ya kutembelea Bunge. Barua hiyo ni vyema ikaeleza tarehe inayokusudiwa, idadi na madhumuni ya kutembelea Bunge na kutumwa kwa anwani ifuatayo:

Katibu wa Bunge

S.L.P 941

DODOMA

Au

Katibu wa Bunge

S.L.P 9133

DAR ES SALAAM



Ofisi ya Bunge hujibu barua zote za maombi ya kutembelea Bunge. Maombi yote yatakayozingatia utaratibu hukubaliwa kama yalivyo, isipokuwa tu kama maombi mengi yamegongana tarehe na idadi ya watu ni kubwa kuzidi uwezo wa maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya wageni. Ikitokea hivyo, ushauri hutolewa kwa baadhi ya waombaji kupanga tarehe nyingine muafaka.

Ukaaji ndani ya Bunge

Kanuni ya 140 ya Kanuni za kudumu za Bunge inaelekeza kuwa, Spika ataweka utaratibu maalumu wa Ukaaji wa Wabunge ndani ya Bunge bila Kuathiri mpangilio ufuatao:

  • Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni (Waziri Mkuu) anakaa kiti cha kwanza akifuatiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mawaziri upande wa kulia wa Spika
  • Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni anakaa kiti cha kwanza akifuatiwa na Wasemaji Wakuu wa Kambi ya Upinzani, upande wa kushoto wa Spika.
  • Endapo hakuna Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani aliyechaguliwa na chama chenye haki ya kuchagua Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni lakini Wabunge wa upinzani wapo, basi Wabunge hao watakaa upande wa kushoto wa Spika.

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's