Parliament of Tanzania

Timu ya Bunge yaahidi kufanya vizuri katika mashindano ya michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki

TIMU ya Bunge Sport Club imeahidi kufanya vizuri katika mashindano ya michezo ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayotarajiwa kuanza Desemba mosi mwaka huu Jijini Bujumbura nchini Burundi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, wakati wa maandalizi kwa ajili ya mashidano hayo katika Uwanja wa jamhuri Jijini Dodoma, Kocha Mkuu wa timu ya Soka, Venance Mwamoto amesema kuwa wamejiandaa kufanya vizuri katika mashindano hayo na kuwatoa kimasomaso Watanzania.

Mwamoto ambaye ni Kocha mchezaji na Mbunge wa Kilolo, alisema kwa sasa timu za Taifa zimekuwa zikifanya vibaya katika mashindano mbalimbali hivyo akawataka Watanzania kuamini kwamba timu ya Bunge la Tanzania itawafuta machozi kwa kufanya vizuri.

“Hivi karibuni tumefanya vibaya kwa timu yetu ya Taifa kwa kufungwa na Lesotho pia timu ya Vijana nayo ilipoteza mategemeo yapo kwetu niwaahidi Watanzania hatutawaangusha,”alisema Mwamoto.

Mwamoto ambaye amewahi kuzichezea timu za Majimaji ya Ruvuma,RTC Kagera na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ miaka ya nyuma,alisema kwa sasa timu hiyo ina majeruhi wawili ambao ni Mbunge wa Rufiji Mohammed Mchengerwa na Sixtus Mapunda ambaye ni Mbunge wa Mbinga Mjini .

Kwa upande wake,Kocha wa timu Netiboli, Eleonora Mongi alisema maandalizi yanaendelea vizuri na kwamba wanauhakika wa kutetea ubingwa wa mashindano hayo kutokana na maandalizi ya kueleweka waliyoyafanya.

Kwa upande wa timu ya Mpira wa Wavu inayojifua katika Viwanja vya Chuo cha Biashara CBE Kocha amesema kuwa timu zote za Wanawake na Wanaume wameahidi kufanya vizuri katika michuano hayo.

Nahodha wa timu ya Mpira wa Wavu ya Wanaume Mheshimiwa Aeshi Hilary amesema wachezaji wa mpira wa wavu wako vizuri na amewaahidi wabunge na watanzania kwa ujumla kuwa wanaenda kuchukua Ushindi.

Naye Nahodha wa Timu ya Mpira wa Wavu ya Wanawake Mheshimiwa Jesca Kishoa amesema wachezaji wamejipanga kisawaswa kuhakikisha wanarejea nchini wakiwa na ushindi.

Timu ya Bunge Sports Club imeweka kambi ya zaidi ya wiki tatu pamoja na kucheza michezo kirafiki ili kuangalia mapungufu ya timu kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's