Parliament of Tanzania

TANZIA

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Y. Ndugai (Mb), anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mhe. Mchungaji Dkt. Getrude Rwakatare kilichotokea Jijini Dar es Salaam alfajiri ya leo Jumatatu tarehe 20 Aprili, 2020.

“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mhe. Rwakatare. Natoa pole kwa wafiwa wote wakiwemo familia ya marehemu, ndugu, jamaa, Waheshimiwa Wabunge na Waumini wa Kanisa la Mlima wa Moto (Mikocheni B Assemblies of God). Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Mhe. Spika.

Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya Marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amina.

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's