United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge umeanza tarehe 6
Novemba, 2018 na unatarajiwa kuahirishwa tarehe 16 Novemba, 2018 ambapo shughuli
ya kwanza iliyofanyika ni Wabunge wateule wanne kuapishwa. Wabunge hao ni;-
(i)
Mhe. Timotheo Paul Mnzava (Jimbo la Korogwe Vijijini –
(CCM)
(ii)
Mhe. Mwikwabe Mwita Waitara (Jimbo la Ukonga – (CCM)
(iii) Mhe.
Julius Kalanga Laizer (Jimbo la
Monduli – (CCM)
(iv)Mhe. Zuberi Mohammed
Kuchauka (Jimbo la Liwale – (CCM).
Akizungumza na Waandishi wa Habari siku moja kabla ya kuanza
kwa Bunge Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (Mb) amesema kuwa shughuli nyingine zinazotarajiwa
kufanyiwa kazi katika mkutano huu ni kama ifuatavyo;-
1.
Maswali
Kuhusu
Maswali yatakayoulizwa Bungeni, Mhe. Spika amesema kuwa Maswali 125 ya Kawaida
yanatarajiwa kuulizwa na Wabunge. Aidha, wastani wa Maswali 16 ya papo kwa papo
kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu yanatarajiwa kuulizwa siku za Alhamisi tarehe 8 na
15 Novemba, 2018.
2.
Kamati
ya Mipango
Kwa mujibu
wa Mhe. Spika madhumuni makubwa ya
Mkutano huu wa Bunge ni kwa ajili ya Waheshimiwa Wabunge kujadili na kuishauri
Serikali kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na
Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020.
“Katika
Mkutano huu sehemu kubwa ya mijadala ya Wabunge ni kuhusiana na huu Mpango
utakaowasilishwa Bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango,” alisema Mhe. Ndugai.
Aidha,
Mhe. Spika aliongeza kuwa Mpango huu utajadiliwa kuanzia tarehe 6 hadi 12
Novemba, 2018.
Kwa
mujibu wa Kanuni ya 94 ya Kanuni za Bunge, Toleo la Januari, 2016 Bunge litakaa
kama Kamati ya Mipango ili kukidhi matakwa ya Ibara ya 63 (3) (c) ya Katiba kwa
kujadili na kuishauri Serikali kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Taifa
unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali katika Mwaka wa Fedha husika.
3.
Miswada
ya Sheria ya Serikali
Mhe.
Ndugai amesema pia kuwa katika Mkutano huu wa kumi na Tatu Serikali itawaailisha
Bungeni Miswada ya Sheria ifuatayo ambayo itasomwa kwa mara ya kwanza:-
(i)
Muswada
wa Sheria ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Mwaka 2018;
(ii)
Muswada
wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 4) wa Mwaka 2018; na
(iii)
Muswada
wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa Mwaka 2018;
(iv)
Muswada
wa Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania wa Mwaka 2018; na
(v)
Muswada
wa Sheria ya Mamlaka ya Usimamizi wa Nchi Kavu wa Mwaka 2018.
Kwa
upande mwingine Mhe. Spika amesema kuwa, Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za
Fedha wa Mwaka 2018 (The Microfinance
Bill, 2018) ambao umewasilishwa kwa hati ya dharura utasomwa
Mara ya Kwanza na hatimaye kupitishwa na Bunge katika Mkutano huu.
4.
Maazimio
Spika
Ndugai amesema pia kuwa Serikali imewasilisha Maazimio yafuatayo kwa ajili ya
kufanyiwa kazi na Bunge:-
(i)
Azimio la kuridhia Itifaki ya Maendeleo ya Nchi za
Kusini mwa Afrika kuhusu kulinda Hatimiliki za Wagunduzi wa Aina Mpya za Mbegu
za Mimea (Protocol for Protection of New
Varieties of Plant [Plant Breeder’s Rights] in the Southern African Development
Community – SADC);
(ii)
Azimio la kuridhia Mkataba wa Kimataifa wa Kuzuia
Matumizi ya Silaha za Kibaiolojia na Sumu [Convention
on Prohibition of Development, Production and Stockpiling of Bacteriological
(biological) and Toxin Weapons and on Destruction – BTWC]; na
(iii) Azimio la Kuridhia Mkataba wa Takwimu wa Afrika (African Charter on Statistics).