Parliament of Tanzania

Kamati za Kudumu za Bunge zaanza kukutana Mjini Dodoma

Kamati za Kudumu za Bunge zimeanza kukutana leo Jumatatu tarehe 15 hadi tarehe 27 Januari, 2017 Mjini Dodoma kutekeleza majukumu ya kibunge kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kumi wa Bunge uliopangwa kuanza tarehe 30 Januari 2018.

Katika kipindi cha vikao hivyo, shughuli zilizopangwa kutekelezwa na Kamati ni kama ifuatavyo:

a) ZIARA ZA UFUATILIAJI

Katika utekelezaji wa majukumu yake, Kamati Tatu (3) zitafanya ziara za ufuatiliaji katika maeneo mbalimbali nchini. Kamati hizo ni Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa - LAAC, Kamati ya Hesabu za Serikali - PAC pamoja na Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utaliii.

b) UCHAMBUZI WA MISWADA MBALIMBALI NA KUPOKEA MAONI YA WADAU

Kamati Tatu (3) za Kisekta zitakuwa na shughuli za uchambuzi wa Miswada ya Sheria kama ifuatavyo;

i) Kamati ya Katiba na Sheria itachambua na kujadili Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 5 wa Mwaka 2017 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2017]. Kamati hiyo pia itakuwa na kikao cha kupokea maoni ya Wadau kuhusu Muswada huo siku ya Jumanne tarehe 16 Januari, 2018 kwenye ukumbi uliopo katika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma kuanzia saa tatu kamili (3:00) asubuhi hadi saa Tisa (9:00) Alasiri.

ii) Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii itachambua na kujadili Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Mwaka 2017 [The Wildlife Conservation (Amendment) Bill, 2017]. Kamati hiyo pia itakutana na kupokea maoni ya Wadau kuhusu Muswada huo siku ya Jumanne tarehe 16 Januari, 2018 kwenye ukumbi uliopo katika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma kuanzia saa tatu kamili (3:00) asubuhi hadi saa Tisa (9:00) Alasiri.

iii) Kamati nyingine ni Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ambayo itachambua Muswada wa Sheria ya Hifadhi ya Jamii wa Mwaka 2017 (The Public Service Security Fund, Bill, 2017) na itakuwa na vikao vya kupokea maoni ya wadau kuhusu Muswada huo siku ya tarehe 18 Januari, 2018 kwenye ukumbi uliopo katika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma kuanzia saa tatu kamili (3:00) asubuhi hadi saa Tisa (9:00) Alasiri.

Wadau wote katika Miswada iliyotajwa hapo juu wanakaribishwa kufika mbele ya Kamati kutoa maoni yao katika tarehe na muda uliotajwa.

c) KUPOKEA TAARIFA ZA KIUTENDAJI WA WIZARA

Kamati Tisa (9) za kisekta zitaendelea kupokea Taarifa za kiutendaji wa Wizara zinazosimamiwa na Kamati hizo kwa mujibu wa Kifungu cha 7 (1) (c) na (d) cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo Januari, 2016.

Aidha, Kamati ya Bajeti pamoja na shughuli nyingine itapokea maoni ya wadau wa Utalii kuhusu Mwenendo wa shughuli za Utalii baada ya kuanzisha utozaji wa VAT kwenye shughuli za Utalii.

2.0 KUMBI ZITATAZOTUMIKA

Tofauti na hapo awali kwa sasa Kamati zote zitakutana kwenye kumbi zilizopo katika Ofisi ya Bunge mjini Dodoma. Uamuzi huu umefikiwa baada ya kubaini yafuatayo;

· Ukubwa wa gharama kwa kukodi kumbi nje ya Ofisi ya Bunge,

· Usumbufu kwa Wabunge kutokana na umbali wa kumbi zilipo,

· Ugumu wa uratibu kutokana na kutawanyika kwa kumbi,

· Usumbufu kwa wadau wanaoalikwa kwenye kamati na;

· Changamoto ya Utoaji wa huduma muhimu zinazofanikisha shughuli za Kamati.

Hivyo, changamoto zote hizo zinatatuliwa kwa Vikao vya Kamati zote kufanyika katika eneo moja la Ofisi ya Bunge ambapo huduma zote muhimu kiutawala, utaratibu, afya, ulinzi na ustawi wa Wajumbe zitapatikana kwa urahisi, ubora, uharaka na zaidi kupunguza gharama na kuongeza ufanisi.

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

View All MP's