Parliament of Tanzania

Kamati za kudumu za Bunge zaanza kukutana Jijini Dodoma

Kamati za Kudumu za Bunge zimeanza kukutana Jumatatu tarehe 11 hadi 31 Machi, 2019 Jijini Dodoma kutekeleza majukumu ya kibunge kabla ya Mkutano wa Kumi na Tano wa Bunge uliopangwa kuanza tarehe 02 Aprili, 2019.

Shughuli zitakazotekelezwa na Kamati hizo ni pamoja na:

a) KUPOKEA WASILISHO LA SERIKALI KUHUSU KIWANGO CHA UKOMO WA BAJETI

Katika kipindi hicho cha vikao vya Kamati za Bunge, siku ya tarehe 12 Machi 2019, Wabunge watapokea Wasilisho la Mapendekezo ya Serikali kuhusu Mpango na Kiwango cha Ukomo wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 kwa mujibu wa Kanuni ya 97 ya Kanuni za Bunge Toleo la Januari, 2016.

b) KUFANYA ZIARA ZA UKAGUZI WA MIRADI

Kamati zitafanya ziara za ukaguzi wa miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha katika Bajeti ya mwaka 2018/2019 kwa mujibu wa Kanuni ya 98(1) ya Kanuni za Bunge Toleo la Januari, 2016. Kamati zitakagua miradi ya uwekezaji liyotekelezwa na Serikali kupitia Mashirika ya Umma. Aidha, Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) zitafanya ziara za ukaguzi wa miradi mingine iliyotekelezwa na Serikali ili kulinganisha matokeo ya utekelezaji na thamani halisi ya fedha za Umma zilizotumika katika miradi hiyo.

c) KUFANYA UCHAMBUZI WA BAJETI

Katika vikao hivyo pia Kamati zitafanya uchambuzi wa Taarifa za Utekelezaji wa Bajeti za Wizara inazozisimamia kwa Mwaka wa Fedha unaoishia 2018/2019 kwa ajili ya kufanya ulinganisho kuhusu makadirio ya matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 kwa mujibu wa Kanuni ya 98(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016.

d) KUFANYA UCHAMBUZI WA TAARIFA ZA UWEKEZAJI

Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) itafanya uchambuzi wa Taarifa za Uwekezaji uliofanywa na Serikali kupitia Mashirika ya Umma kwa mujibu wa Kifungu cha 12 cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Bunge Toleo la Januari, 2016.

e) UCHAMBUZI WA SHERIA NDOGO

Kamati ya Sheria Ndogo itafanya uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa wakati wa Mkutano wa Kumi na Nne Bunge kwa mujibu wa Kifungu cha 11 cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Bunge Toleo la Januari, 2016Bofya hapa kusoma ratiba zote za Shughuli za Kamati za Bunge ikiwa ni pamoja na maeneo ambayo Kamati hizo zitafanya ziara

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's