Parliament of Tanzania

Bunge lapitisha Miswada ya sheria za ulinzi wa Maliasili za Taifa

Bunge limepitisha Miswada ya Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili ya mwaka 2017 na Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba inayohousu Rasilimali na Maliasili za Nchi ya mwaka 2017.

Miswada hiyo iliyoletwa Bungeni kwa Hati ya Dharura iliwasilishwa Bungeni na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi na kujadiliwa kwa siku moja.

Kabla ya kuwasilishwa Bungeni Miswada ya Sheria hizo ilijadiliwa na Kamati ya Bunge ya Pamoja huku wadau mbalimbali wakipata fursa ya kutoa maoni yao.

Akizungumza mara baada ya kupitishwa kwa Sheria hizo, Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai alisema Bunge limeshafanya kazi yake kwa miswada hiyo kwa hatua zake zote na kwamba kilichobaki ni kupelekwa kwa Mheshimiwa Rais ili iweze iliweze kusainiwa kwa mujibu wa Ibara ya 97 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

“Niwapongeze sana Wabunge mliofanya kazi bila kuchoka,pongezi kwa Kamati ya Pamoja ya Bunge,Chini ya Mwenyekiti Mheshimiwa Doto Biteko, Miswada ilipelekwa kwenye Kamati Nne, jambo ambalo katika Bunge la 11 ni mara ya kwanza, zaidi ya Wabunge 100 waliipitia kifungu kwa kifungu na hatua kwa hatua,” alisema.

Mheshimiwa Spika pia aliwapongeza wadau wote waliofika Bungeni Dodoma kwa ajili kutoa maoni yao yaliyosaidia kuboresha muswada hiyo.

“Naipongeza pia Serikali na kipekee Mheshimiwa Kabudi kwa ushiriki wake mkubwa katika jambo hili, jinsi ambavyo yeye na timu yake wamefanya kazi usiku na mchana,” alisema

“Kuna maeneo ambayo Serikali ilileta Jedwali la Marekebisho maana yake ni kwamba imeyakubali maoni yaliyotolewa na imeboresha hii ni ‘spirit’ nzuri kwa Serikali, tunaipongeza kwa kukubali kuwasikiliza Wabunge na Wadau,” aliongeza Spika

Aidha, alisema Miswada hiyo miwili imeliingiza Bunge la 11 katika hisrtoria ya kipekee na kwamba kama spika wa Bunge anajisikia faraja kwa kuingia katika historia hiyo mpya ya kuangalia maliasili ya nchi kwa kuweka sheria ya Watanzania kuimiliki na kuweka taratibu za mikataba zilizopigiwa kelele kwa muda mrefu.

“Hatua hii ni kubwa tunaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano, kama tukiona kuna matatizo, Serikali ipo na sisi Wabunge tupo,tutakaa na kuona jinsi ya kuweka vizuri zaidi,” alisema.

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's